June 18, 2019


Watu 29 wamejeruhiwa baada ya lori kugonga treni jijini Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protas Katambi, amesema leo asubuhi Jumanne Juni 18, 2019, kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 5.30 usiku.

Amesema ametoa maagizo kwa vyombo vya usalama kumsaka dereva wa lori ambaye inasemekana aliruka kutoka kwenye lori baada ya ajali hiyo kisha kutokomea kusikojulikana.

Shughuli ya kuondoa mabehewa ya treni inaendelea huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la tukio na polisi waliokuwa na silaha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic