June 18, 2019


MLINZI wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars), Joash Abong’o Onyango,  amezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha yake kusambaa akiwa akiwa na mwonekano mpya wakati wa maandalizi ya fainali za AFCON 2019.

OnyangoliJanuari 31, 1992, hivi sasa ana umri wa miaka 27, lakini baadhi ya wadau katika mitandao hiyo wamedai kuwa muonekano wake na umri anaotajwa haviendani kwani ni mzee tofauti na miaka yake ilivyo.

Mchezaji huyo wa Gor Mahia, ameweka mwonekano ambao wachezaji mbalimbali wa Afrika waliwahi kuonekana hivi kama El Hadji Diouf wa Senegal na Rigobert Song wa Cameroon ambao pia walionekana hivyo kwenye mashindano kama hayo.

Harambee Stars wataondoka leo nchini Ufaransa walikopiga kambi na kuelekea Misri. Onyango ni miongoni mwa wachezaji tegemezi wa kocha Sebastien Migne, hasa baada ya kuumia kwa beki Brian Mandela. Kenya wapo Group C na Algeria, Senegal na Tanzania.

Harambee Stars watakipiga na Algeria, Juni 23 wakati siku hiyo, Taifa Stars itacheza na Senegal.

1 COMMENTS:

  1. Ana mwonekano kama wa Meddie Kagere!!!Kikubwa ni uwezo uwanjani mvi majaliwa ya Mwenyezi Mungu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic