June 24, 2019


KIGOGO wa TP Mazembe yupo Jijini Dar es Salaam kufanya mazungumzo ya awali na Simba na Yanga. Si hao tu pia wanazungumza na wakala wa straika wa Serengeti Boys, Kelvin John ‘Mbappe’.

Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga ni kwamba, Mazembe wanawataka wachezaji hao watatu kwa mpigo lakini mazungumzo yako kwenye hatua za awali.

Habari zinasema kwamba tayari wameshazungumza na Yanga na Simba kwa nyakati tofauti na leo huenda wakafikia muafaka na wiki ijayo wakamaliza dili.

“Wanataka wachezaji wote watatu na wiki ijayo huenda ukasikia habari njema kwani huo usajili unaeza kumalizika na watakuwa wamefikia muafaka,” alidokeza kiongozi mmoja wa Yanga licha kutotaka kutajwa jina lake kwa madai kwamba ishu hiyo ipo kwenye hatua za awali sana.

Fei Toto amekuwa mhimili wa Yanga katika Ligi Kuu msimu uliopita na sasa yupo Taifa Stars kwenye Afcon.

Tshabalala alifanya vizuri na Simba kwenye michuano ya kimataifa msimu uliopita pamoja na ligi ya ndani huku Mbappe akiwa ndiye straika namba moja wa Serengeti Boys na mchezaji anayetajwa kufuata nyayo za Mbwana Samatta.

4 COMMENTS:

  1. Inaonesha kuwa Mazembe ni timu Tajiri inatataka kuwanunua wachezaji kutoka timu masikini zinazohitaji hela

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe sana,maskini ndio waopenda hela,kagere amenunuliwa 150 Sasa anauzwa 500 duh

    ReplyDelete
  3. Shabalala itakuwa ngumu simba nao wanamtaka Na Jana kapigwa lini ya miaka 3 akiwa huko huko Misri kwa kiwango cha jana cha Fei Toto ni vyema aende akaongezewe makali pamoja na huyo Mbambe.

    ReplyDelete
  4. Nyambaf!!!!! kwa uwezo gani walionao hawa wachezaji uliowataja kuweza kusajiliwa na TP Mazembe.Hizi habari zako za kuuza kijigazeti chako tumeshazistukia na kuchoka nazo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic