Kiungo machachari wa Simba, Mnyarwanda Haruna Niyonzima, amevunja ukimya kuwa mpaka sasa uongozi wa timu hiyo haujazungumza naye ishu yoyote ya kuongeza mkataba na kwamba hilo halimtishi kwani ana ofa kibao.
Niyonzima alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita akitokea Yanga, alianza kazi Msimbazi kwa kusuasua kutokana na majeraha kabla ya kuibuka hivi karibuni na kuonyesha kiwango kizuri.
Kwa sasa mkataba wake Msimbazi umemalizika. Akizungumza na Championi Jumamosi, Niyonzima alisema, anapenda kuendelea kucheza Simba licha ya kuwa mkataba wake umekwisha na hajaambiwa lolote na viongozi wa timu hiyo.
Alisema hata kama Simba hawatampa mkataba mwingine haina shida kwani ana ofa nyingi ambazo amezipata. “Mimi ningependa sana kuwepo Simba lakini kwa sasa napata kigugumizi kusema lolote kwa kuwa mkataba umeisha na sijaambiwa lolote na uongozi.
“Watu wajue kuwa hapa (Tanzania) pameshakuwa kama nyumbani na nisingependa kuondoka, lakini itategemea uongozi unasemaje maana mwisho wa siku namaliza mkataba kwa hiyo siwezi kung’ang’ania kama wao hawanihitaji,” alisema Niyonzima.
Wachezaji wa Simba wanapaswa kuwa makini katika wakati huu wa usajili hasa baada ya mafanikio waliyoyapata klabu bingwa Africa. Wanatakiwa kuiga mfano wa wachezaji wa Liverpool kwani baada ya kuifikisha Liverpool fainali ligi ya mabingwa msimu uliopita wengi wa mastaa wa Liverpool walitakiwa na vilabu kadhaa vyenye pesa zaidi lakini wachezaji wao walikuwa watulivu zaidi na utulivu wao umekuja kuwalipa msimu huu. Wakati mwengine pesa sio kila kitu katika maisha.
ReplyDelete