June 2, 2019

6 COMMENTS:

  1. Simba walishindwa kutamba mbele ya kikosi cha kuokoteza cha Yanga na kisichokuwa na uongozi thabiti na kilichokuwa na wachezaji wanaocheza na njaa kutokulipwa mishahara yao chini ya Zahera. Sasa Yanga ina uongozi thabiti na wachezaji waliofuatiliwa na kocha wao na kujiridhisha kuwa wapo vizuri na hapana shaka ni kikosi kitakachokuwa kinatimiziwa mahitaji yao kwa wakati msimu ujao. Sasa kama Simba watauchukulia usajili wa Yanga poa basi kuna uwezekano mkubwa Yanga kuja kubeba taji la ligi kuu na kumgaragaza mnyama mchana kweupe. Kwa ninavyoamini mimi kama Yanga hii ya msimu huu ingekuwa Simba wasingehangaika kufanya usajili wowote labda wachezaji wawili wa tatu lakini Zahera ameonesha kuwa sio mtu wa mchezomchezo kwa kukifumua kikosi karibu chote cha Yanga na kuunda kikosi kazi cha maana mwakani. Hapana shaka Zahera anaiunda Yanga kwa kutizama madhaifu ya Simba yapo wapi na kama Simba watabweteka na kuvimba kichwa kuwa wana kikosi kizuri basi kitakachokujakuwatokea mbele ya Yanga mwakani hawataamini macho yao. Ukiiangalia Simba unaona kabisa ni timu yenye mapungufu kadhaa wa kadhaa na ni ya muda mrefu lakini wamekuwa na kasi ya konokono kutafuta wachezaji wa kuziba mapungufu hayo.Licha ya sababu yakwamba Simba wanasubiri ripoti ya kocha wao ili wafanye usajili lakini unakaa ukijiuliza Zahera aliwezaje kukamilisha usajili wa kikosi kizima kipya cha Yanga kabla Afcon kuanza mara tu baada ya kumalizika ligi na kuwaacha Simba wakijiuma meno bila ya kusajili hata mchezaji mmoja ambao kama inavyosemekana Simba wanahitaji kusaini wachezaji wanne lakini kwa inavyoonekana ligi kuu inaweza kuanza mwakani bado Simba hawajakamilisha idadi hiyo ya wachezaji wanaowahitaji.Unajua wakati mwengine sisi watanzania tupo very slow katika ufanisi na ndipo tunapopigiwa na wageni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. 1.Kusajili na kuweza kuwalipa stahiki zao za kimkataba ni mambo mawili tofauti.
      2.Malengo ya yanga ni tofauti kabisa na yale ya simba
      3.Vuta subira hadi dirisha la usajili litakapofungwa kisha ulinganishe ubora wa vikosi.
      4.Mafanikio ya mpira hutegemea mipango madhubuti+ pesa...sio siasa.
      5.Unavyosema simba ilishindwa kuifunga yanga unaongea kwa kipimo kipi?...msimu huu mmepoteza points ngapi kwa simba?

      Delete
  2. Yanga inasajili kwa ligi kuu na Simba inasajili kwa ajili ya Champions League Africa. Hiyo ndio tofauti.

    ReplyDelete
  3. Aussems sio mgeni Hiyo ni wishfull thinking. Sijaona mchezaji yeyote wa maana aliyesajiliwa na Yanga mpaka sasa licha ya kupoteza wachezaji wawili walioibeba msimu uliopita. Makambo na Ajibu.Upenzi ni upofu .Time will tell.

    ReplyDelete
  4. Kwa Kahata Simba imeliwa, ni mchezaji wa kawaida sana hana tofauti na tulionao ndani. Tunatatizo katika scouting.

    ReplyDelete
  5. Simba haikuwa na sababu ya kipiga kelele Kwa kila wakifanyacho kwasababu hiyo ni alama ya hofu. Wale nyota waliotesa na kuleta mafanikio makubwa walipatikana bila ya kujitangaza na kupiga makelele na mwaka huu ni Zaidi tena bila ya papara na tutasitukia tu na hii ndio kujiamini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic