June 15, 2019


MABINGWA wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo Simba, msimu wa 2017/18-na 2018-19 wamepata mualiko wa kucheza mchezo wa kirafiki Juni 21 dhidi Gwambina FC.

Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kuzindua uwanja wa timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza yenye lengo la kuzindua uwanja wa Gwambina uliopo Mwanza.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema ni heshima kubwa kucheza mchezo wa kirafiki ambao ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja.

"Timu itatua Mwanza kwa ndege tarehe 20 Juni, 2019 na mechi itapigwa Uwanja wa Gwambina tarehe 21 Juni, 2019 dhidi ya Gwambina FC. 

"Wachezaji wapya wa ndani watachezea Simba kwa mara ya kwanza. Wanasimba wa Kanda ya Ziwa jiandaeni kuipokea timu yenu," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic