Leo timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itaingia uwanjani katika mchezo wa pili wa majaribio dhidi ya Zimbabwe, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa El Sekka El Hadid jijini Cairo majira ya saa 2:00 usiku.
Stars imeweka kambi nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afcon ambayo inatarajiwa kuanza Juni 21 huu unakuwa mchezo wa pili na mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Misri.
Stars ipo katika kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya, ambapo itacheza mchezo wake wa kwanza wa makundi Juni 23 dhidi ya Senegal.
Stars imepata nafasi hiyo baada ya miaka 39 kupita, ambapo mara ya mwisho kushiriki ni mashindano ya mwaka 1980 nchini Nigeria.
Wakati huo Taifa Stars iliishia katika hatua ya makundi, ambapo safari hii inahitaji kujiandaa zaidi ili iweze kutengeneza historia mpya kwa kuvuka hatua ya makundi.
Wajikaze mpira wa sasa hakuna cha uanda dog ni kupambana.Japo ni mechi ya kirafiki lakini nilimshuhudia Uganda akimgaragaza Ivory coast mchana kweupe.
ReplyDeleteIlibidi wapate test matches kiasi tatu kabla hawajaondoka mambo yangezidi kunoga, juu ya hivo tunawaombea kila la kheri
ReplyDelete