OFISA Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wachezaji na uongozi wa timu kwa sasa wanafuraha baada ya kuwang'oa vigogo TP Mazembe.
Jana Azam FC iliwatoa mashabiki wa Tanzania kimasomaso kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali michuano ya Kagame.
"Haikuwa kazi nyepesi kwani wao walianza kutufunga, wachezaji walitambua kwamba wanakazi ya kupeperusha Bendera ya Tanzania ndio maana walipambana.
"Kwa sasa furaha ni kama yote maana kila hatua ambayo tunapita ni ngumu hivyo tumetinga hatua ya nusu fainali tunajipanga kufanya vema, shukrani kwa mashabiki pia" amesema.
Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wanasubiri mshindi wa mchezo kati ya APR na AS Maniema utakaopigwa leo ambaye watacheza nae hatua ya nusu fainali.

0 COMMENTS:
Post a Comment