July 18, 2019


Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mechi za mashindano makubwa.

Mabadiliko hayo ni kuanzia msimu ujao wa 2019/20 ambapo limepitisha maamuzi ya mechi za fainali kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) na klabu bingwa Afrika (CAF Champions League).

Kilichobalika ni kuchezwa mechi moja tu badala ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.

Aidha, mechi hizo za fainali zitachezwa katika uwanja huru kwa timu zote zinazofika fainali.

Mabadiliko haya ni sawa na namna mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na UEFA Europa League namna yanavyofanyika.

9 COMMENTS:

  1. UEFA wanataja mapema uwanja siyo huru as such.Mfano CAF wakisema mwaka 2020 CAF CL fainali inachezwa Daresalaam (bola kujua nani ataingia fainali) halafu timu yotote ya Tanzania ikaingia fainali utaita uwanja huru.?UEFA wanautangaza mapema

    ReplyDelete
  2. Wawe makini wasije wakafanya majongoo kwenye uwanja huru.

    ReplyDelete
  3. Hapo sawa lakini suala la kijiografia lizingatiwe ili lisije likawa rafiki kea timu moja cha msingi mazingira ya uwanja yaathiri timu zote mbili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic