July 18, 2019


Mchezaji wa zamani wa Lipuli na sasa Yanga, Ally Sonso anayecheza nafasi ya beki, ameibuka na kueleza hana kinyongo kuhusiana na kutoitwa katika kikosi cha Taifa Stars.

Katika kikosi cha wachezaji kilichoitwa na Kocha Mrundi Ettiene Ndayragije hivi karibuni baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo kutokana na aliyekuwa Kocha Emmanuel Amunike kufukuzwa kazi, Sonso hajajumuishwa licha kuwa sehemu ya kikosi kilichokuwa AFCON 2019.

Kuachwa kwa Sonso kumefanya aseme hana shida na Kocha kwani ni maamuzi yake kama Mwalimu na hawezi kulalamika wala kuhoji.

Sonso ambaye yuko kambini na kikosi cha Yanga mjini Morogoro ameeleza kuheshimu maamuzi na Ndayiragije na akiitakia kheri Stars kuelekea kufuzu mashindano ya CHAN ambayo yatafanyika Cameroon mwakani.

Stars itaanza kibarua cha kuwania tiketi ya mashindano hayo Julai 28 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na mechi ya marudiano itakuwa Agosti 4 huko Kenya.

3 COMMENTS:

  1. Ndayragije anajua huyu sio defender ila ni uchochoro kwa hio ni sawa tu kwa kuachwa.

    ReplyDelete
  2. ukubali usikubali, maamuzi ya kocha yatabaki hivyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic