ARSENAL ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na nyota wa Gremio raia wa Brazil, Everton Soares.
Winga huyo mwenye miaka 23 ameongeza thamani yake baada ya kuonyesha maajabu kwenye michuano ya Copa America na amezivutia pia timu nyingi ikiwemo Everton.
Hata hivyo kwa sasa yupo kwenye hatua za mwisho kutua Arsenal baada ya washika bunduki hao kukubaliana na Gremio kuhusu suala la mkwanja wa usajili.
Wilfried Zaha alikuwa ni chaguo namba moja kusajiliwa na Arsenal msimu huu ila dau la milioni 80 ambalo mabosi wa Crystal Palace wanalitaka limewakimbiza washika bunduki hao ambao bajeti yao ilikuwa chini ya pauni milioni 70.
Everton, anatajwa kuwa mbadala wa Zaha baada ya kupendekezwa na meneja wa kikosi hicho Unai Emery na tayari wamemtuma daktari amfanyie vipimo huku mke wake akithiitisha kwamba ameanza kujifunza lugha ya kiingereza,
0 COMMENTS:
Post a Comment