July 19, 2019


WAKATI Jeshi zima la Simba likiwa linaendelea kujifua kwenye kambi yake nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa sehemu hiyo ambayo Simba wameweka makazi paliwahi kukaliwa na timu ya taifa ya England wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

Simba wamekimbilia Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara sambamba na michuano ya kimataifa ambapo katika msafara wao huo, yupo Ibrahim Ajibu aliyejiunga nao hivi karibuni akitokea Yanga.

Kikosi hicho kinachofundishwa na Mbelgiji Patrick Aussems, kimeweka kambi katika Mji wa Rustenburg, Afrika Kusini ambapo pia mabingwa wa zamani wa nchi hiyo, Orlando Pirates wapo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori ameliambia Championi Ijumaa, kuwa kambi hiyo ni bora kwani iliwahi kukaliwa na timu ya taifa ya England wakati walipokuwa wakishiriki Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

“Watu wasione kwamba tumeweka kambi kule Afrika Kusini wakadhani kwamba ni kambi tu ya kawaida. “Mahali ambapo sisi tumeweka kambi, England waliwahi kukaa pale wakati wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010.

“Hilo eneo ni zuri na lina vifaa vyote ambavyo mwalimu amevitaka kwa ajili ya kujenga stamina kwa timu pamoja na mazoezi mengine,” alisema Magori. Miongoni mwa nyota wa England ambao walikaa katika kambi hiyo waliopo Simba kwa sasa ni Wayne Rooney, John Terry, Steven Gerrard, Frank Lampard na Peter Crouch.

8 COMMENTS:

  1. Ishu siyo kambi ya hela ishu Uwezo wa kucheza mpira mambo hata kwenye unaweza kuweka Kwa meli kubwa lakini kama uwezo wa kucheza hakuna ni shida,haichezi kambi

    ReplyDelete
  2. Kambi hata baharini unaweza weka ila si tunachotaka mpira Mkubwa siyo kbi kubwa

    ReplyDelete
  3. Kambi hata baharini unaweza weka ila si tunachotaka mpira Mkubwa siyo kbi kubwa

    ReplyDelete
  4. Povu la nini? Msipaki basi mkikutana nao chezeni mpira.

    ReplyDelete
  5. Je England ilivyokaa pale,ilichukua kombe la dunia?

    ReplyDelete
  6. Hiyo kambi anakaa Ajib peke yake au?kama ni peke yake basi kichwa cha habari kipo sahihi lakini kama ni timu nzima ulipaswa kuandika timu ya Simba

    ReplyDelete
  7. Magori ni mshamba sana,majivuno ya kambi ghali eti baadhi ya wachezaji wa england kwa kuwataja majina imekuwa sifa mbona shoga maarufu duniani yupo kwny kambi hiyo

    ReplyDelete
  8. Magori ni mshamba sana,majivuno ya kambi ghali eti baadhi ya wachezaji wa england kwa kuwataja majina imekuwa sifa mbona shoga maarufu duniani yupo kwny kambi hiyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic