SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania, amesema kuwa atashirikiana na bosi wake mkubwa Ettiene Ndayiragije kuifanya Stars kufanya maajabu michuano ya Chan.
Stars itamenyana na Kenya, Julai 28 uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa kufuzu michuano ya Chan inayoshirikisha wachezaji wa ndani.
Matola amesema kuwa ana imani na wachezaji ambao wamewateua kwa kushirikiana na kocha mkuu watafanya mambo mengi makubwa.
"Taifa ni letu sote nasi tuna kazi ya kufanya kuona kwamba tunatisha hivyo kikubwa ni ushirikiano na walimu wenzangu pamoja na timu kiujumla," amesema Matola.
Mwingine mzawa ambaye amepata shavu la kuionoa Stars baada ya Emmanuel Ammunike kupigwa chini ni Juma Mgunda.
Huu ni muunganiko wa makocha wenye ufahamu wa kina wa wachezaji wetu wa ndani na kama wataaminiwa na kuwezeshwa kikamilifu basi hakika tunaweza kuwa na mwanzo mzuri wa kuanzia kwa Taifa stars ya 2021 Afcon.
ReplyDelete