EXCLUSIVE: GADIEL MICHAEL AFUNGUKA JUU YA KUSAINI SIMBA
Beki wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael, amekanusha taarifa zilizozagaa kuwa amesaini mkataba na Simba na kwamba hajafanya mawasiliano yoyote na klabu hiyo.
Amesema suala la kuongeza mkataba na klabu yake ya sasa ya Yanga litakamilika siku chache zijazo baada ya kurejea kutoka kwenye mashindano ya ubingwa kwa nchi za Afrika (AFCON) yanayofanyika Misri.
Beki huyo amefunguka kufuatia kuzuka kwa tetesi ambazo hata wanachama na mashabiki wa Yanga zimewashtua.
Ikumbukwe hivi karibuni ilielezwa kuwa Yanga na Gadie wapo kwenye mazungumzo ya kumalizana na mchezaji huyo tayari kwa kumuongezea mkataba.
Licha ya Gadiel kukanusha, bado kuna taarifa za ndani kutoka Simba zinazoleleza kuwa mabosi wa klabu hiyo wapo kwenye mchakato wa kupata saini yake kuelekea msimu ujao.
Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!
ReplyDelete