July 3, 2019


Kocha wa timu ya wanawake ya Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni ambao wamesajiliwa na Simba, wataibeba timu hiyo kimataifa ila ndani ya Ligi Kuu Bara itakuwa pasua kichwa.

Kwa sasa tayari Simba imemalizana na wachezaji wanne wa kigeni ambao wana uhakika wa kuonyesha makeke yao msimu ujao ikiwa ni pamoja na Wilker Henrique da Silva, Gerson Fraga Viera, Tairone da Silva hawa ni raia wa Brazil wamesaini kandarasi ya miaka miwili na Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman raia wa Sudan ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.

“Wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na Simba watakuwa na msaada mkubwa kwenye michuano ya kimataifa kutokana na ubora wa viwanja ambavyo watacheza pamoja na miundombinu ila kwenye ligi ya ndani watapata taabu.

“Ukweli haujifichi hasa ukizingatia ligi yetu miundombinu bado tatizo hivyo wachezaji wengi watafanya vizuri wakiwa Uwanja wa Taifa ambao una hadhi ya kimataifa wakitoka mkoani itawachukua muda kuzoea mazingira, ila ni somo kwa wazawa nao wanapaswa wapambane wasibweteke,” alisema Mmachinga.

1 COMMENTS:

  1. Ikiwa itafuzu za kitaifa ni timu gani ya nyumbani itayoweza kumdhibiti mnyama?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic