UONGOZI wa KMC umesema kuwa ushiriki wao michuano ya Kagame umewapa fursa ya kujifunza mambo mengi hasa kuelekea kwenye michuano ya kimataifa ambayo itashiriki.
KMC ilialikwa kwenye michuano ya Kagame inayoendelea nchini Rwanda imetolewa hatua za awali baada ya kukusanya pointi nne.
Kwenye kundi A KMC ilishinda mchezo mmoja dhidi ya Rayon Sport na ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Atlabara na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe.
Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa hawajatoka mikono mitupu licha ya kushindwa kutinga hatua ya robo fainali.
"Tumejifunza mengi na mashindano haya yametupa picha halisi ya huko tuendako, ushindani ulikuwa mkubwa mpaka hapa tulipofika si sehemu mbaya, tumepata uzoefu utakaotusaidia kwenye michuano ya kombe la Shirikisho pamoja na Ligi Kuu Bara," amesema.
KMC wameimprove sana from their first game.Wanacheza kitimu,nawanonekana na vipaji wakipata mda wakuzoeana.Abdalah mfuko bonge ya beki...mashindano haya yamewasaidia sana kuweka sawa confidence. Azam fc wanasafari ndefu coz hawaoneshi mipango na win plan...wanachezacheza tuuu....ila wananafasi bado yakubadilika...
ReplyDelete