July 8, 2019



MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Boniface Wambura amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza mwezi Agosti 23 mwaka huu na hakutakuwa na viporo kama msimu uliopita.


Wambura amesema kuwa ratiba ya ligi msimu huu imezingatia kalenda ya michuano ya kimataifa hivyo hakutakuwa na viporo.

"Safari hii hatutakubali kuona timu inaweka kiporo na itambuwe kuwa Bodi ya Ligi haiwabani kwa lolote hivyo ni muda wa kila timu kujipanga ili kufanya vema na kabla ya ligi kuanza mchezo wa ngao ya jamii utakuwa kati ya Simba dhidi ya Azam FC," amesema.

Mchezo wa ufunguzi utakuwa ni kati ya mabingwa watetezi Simba watamenyana na JKT Tanzania uwanja wa Taifa, Agosti 23.

3 COMMENTS:

  1. Ngao ya hisani kwa nini isiwe simba na yanga iwe simba vs azamu?

    ReplyDelete
  2. ngao ya jamii inachezwa na bngwa wa lg kuu vs bngwa wa azam sports federation zaman ilkuwa inachezwa na mshnd wa kwanza vs wa pl wa lg kuu.

    ReplyDelete
  3. Tuna subiri wakalamikaji FC wakiongozwa na Zahera.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic