July 8, 2019

NYOTA wa Simba, Marcel Kaheza ambaye mkataba wake na AFC Leopards ya Kenya alikokuwa kwa mkopo umemalizika kwa sasa ameingia rada za Singida United ambao wanasuka kikosi upya.

Hesabu za Singida United zilikuwa kuipata saini ya mshambuliaji Rashid Juma kutokana na ugumu wa kumpata nyota huyo wameshusha majeshi yao kwa Kaheza.

Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa mpango wa usajili kwa sasa ndani ya Singida United umepamba moto hivyo kama jina la nyota huyo limo kwenye ripoti ya mwalimu watamnasa.

"Tunasajili kwa mapendekezo ya mwalimu hivyo kama atatuambia tumsajili Kaheza tutazungumza naye kwani hakuna kinachoshindikana kikubwa ni kuwa na timu bora itakayoleta ushindani," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Hivi hii hii timu inahitaji ubingwa kweli? Mimi naona hawa wapo kwenye ligi ili kuipa ubingwa Yanga tu.
    Wakisajili wachezaji wazuri wanawasajilia Yanga, huku wenyewe wanahangaika.

    ReplyDelete
    Replies
    1. simba haitakiwi kuwapa wachezaji maana wao wamezoea kuwapa wachezaji yanga

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic