SADIO Mane nyota wa Liverpool amekingiwa kifua na mabosi zake hao juu ya suala lake la kuhitajika na kikosi cha Real Madrid.
Mane ambaye ni nyota pia ndani ya kikosi cha timu ya Taifa cha Senegal ametupia jumla ya mabao matatu na alikosa penalti mbili kwenye michuano ya Afcon iliyomalizika nchini Misri, ilielezwa kuwa anahitajika na Madrid.
Liverpool imesema kuwa haijafanya mawasiliano yoyote na Real Madrid kuhusu Mane licha ya kwamba Rais wa Chama Cha Soka Senegal Saer Seck, kusema Madrid imewasilisha ofa.
0 COMMENTS:
Post a Comment