July 21, 2019


TAYARI mambo yameanza ndani ya Yanga ambapo mashabiki wa sehemu mbalimbali wameanza kujipanga kuelekea kwenye wiki ya Wanachi.

Uongozi wa Yanga umesema kuwa Julai 28 itakuwa ni maalumu kwa wana Yanga wote nchini kufanya masuala ya usafi na kupanda miti.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa lengo ni kuweka historia itakayokumbukwa daima.

Tayari mashabiki wa Yanga wameanza maandalizi ambapo wanachama wa Nzenga walikuwa wakifanya usafi maeneo mbalimbali jambo lililopongezwa na uongozi wa Yanga.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema ni wakati wa mashabiki wa Yanga popote walipo kuungana na wananchi wa Nzega, Tabora kwa kufanya matukio ya kijamii.

Kilele cha wiki ya Mwanachi itakuwa Agosti 4 ambapo kutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya AS Vita ya Congo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic