July 21, 2019

 GADIEL Michael, beki wa kushoto wa Simba  amesema hesabu zake ni kutamba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kufika mbali zaidi ya robo fainali ambayo walifika msimu uliopita.

Gadiel amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga na atakuwa na kazi ya kupambana na Mohamed Hussein 'Tshabalala' ambaye naye ni beki wa kushoto.

 “Nina mambo makubwa nimejiandaa kuyafanya hapa katika timu yangu, kwa hiyo mashabiki wajiandae vizuri kuna vitu vizuri kutoka kwangu nitakavyofanya na nina amini watafurahia.

 “Kwa ninachofikiria kwa kikosi cha Simba tuna matumaini ya kufika mbali katika michuano ya kimataifa kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo walifika hatua ya robo fainali,” amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic