MCHEZAJI MWINGINE TEGEMO YANGA KUTANGAZWA SIMBA LEO SAA SABA
Na George Mganga
Dar es Salaam
Baada ya kufanikisha kumrejesha mchezaji wake wa zamani Ibrahim Ajibu, kuna uwezekano mkubwa wa Simba SC kumtangaza beki Gadiel Michael ambaye ameshamaliza mkataba na Yanga.
Taarifa za ndani zinasema kuwa Michael ameshamalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili tayari kuhudumu kwa misimu miwili ijayo akiwa na uzi mwekundu na mweupe.
Beki huyo ambaye ni sehemu ya nyota walioshiriki michuano ya AFCON na kikosi cha Taifa Stars kilichoondolewa kwa kuchapwa mabao 3-2 na Kenya, ameshindwa kuendelea na Yanga sababu ya kutoelewana juu ya dau la usajili.
Kushindwa kuelewana na Yanga imekuwa kama bahati pekee kwa watani zao wa jadi Simba kumalizana naye ambapo uwezekano wa leo majira ya saa saba za mchana kutangazwa upo.
Usajili wa Michael ndani ya Simba utakuwa ni wa pili kwa mchezaji aliyemaliza mkataba na Yanga katika msimu uliomalizika hivi karibuni (2018/19) kutua Simba ikiwa ni baada ya Ajibu.
Ajibu alitangazwa na Simba wiki jana kwa kuingia mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili ya mwisho mfululizo.
Bado Simba haijatatua tatizo la mabeki wa maana.....beki #3 anatakiwa mtu mwenye uwezo na Uzoefu wa CAF...hawa mabeki (Gadiel & Tshbalala) hawawezi kuzuia forward kali za Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca walioenda juu na wenye kushiba na wenye kasi....tofauti za uchezaji kwa Gadiel na Tshabalala hakuna... NARUDIA tena ni mara mia (100×) Simba tumsajili WALUSIMBI NAMBA 3 KULIKO GADIELI....TUNZA KUMBUKUMBU YA COMMENT HII MTAKUJA KUNIAMBIA.......Simba tunataka mabeki wazoefu na CAF CL....sio mabeki wa kuwazuia lipuli, Ndanda, na alliance!!....huko sie tumeshatoka.....tunadeal jinsi ya kushindana na Esperance, TP Mazembe, Raja Casablanca haswa mechi za ugenini....kwahiyo akina Gadieli hawatatusaidia kitu....hakuna tofauti na Tshabalala!
ReplyDeleteUko sawa lakini kama kocha akaimarisha kiungo na washambuliaji kwa kukaa na mpira muda mwingi ni haki mashambulizi golini kwetu yatapungua na kuwafanya mabeki wapunzike, shida nilyo kuwa naiona Simba ni holding midfielder na winger midfielder wanapoteza mipira kizembe na hawaji kusaidia kukaba, utakuta Chama/Dilunga au Okwi anapoteza mpira kisha anatembea. Defencing inaanza mbele na katikati defenders wanaclear tu, Simba tumekuwa tukakaribisha sana mashambulizi kwani defensive midfielder walikuwa wanazembea au wanachelewa kukaba hadi adui anaingia 18 yard. Nakumbuka 3-5-2 ya Masoud tulikuwa hatufungwi magoli rahisi, Patrick anafundisha 4-4-2 diamond ya kushambulia sana kupitia katikati akiacha kubabia karibu na 18 yard yake kwa kuwa viungo walikuwa wawili ( Kotei na Mkude) na Mkude sio mzuri kukaba ila kuficha mpira na pasi fupi fupi, kazi ya kukaba akabakiziwa Kotei ndio maana hata Kaizer chief waliona atawasidia kwenye kukaba kwani Micho anapenda sana defensive game na kuattack kwa kushtukiza akitumia wingers. So kama Kahata, Shiboub na yule kiungo mbrazili wakiwa na kaliba kama ukabaji na uanzishaji mashambulizi huku Deo Kanda na winger mwingine anasaidia kukaba.
DeleteKweli kabisa aise
DeleteKusajiliwa kwa Gadwel na kurudi Kwa Kapombe kumeshamaliza Tatizo la mabeki
ReplyDeleteKusajiliwa Gadwel na kurudi Kwa Kapombe kumeshamaliza Tatizo la mabeki
ReplyDeleteShida kubwa simba ni mabeki wa kati..sio wa pembeni..km kapombe yule atarudi katika ubora wake cna shaka..wasiwasi wangu mkubwa ni beki wa kati adi sasa cjaona beki wa kati pale simba.wawa kwa umri wake na nyoni bado ni wasiwasi kwakua walicheza mwaka jana na tuliona kilichotukuta mechi za away..uyo mbrazili ndio kabisa cmjui na sitaki kua na imani nae labda nitakapomuona
ReplyDelete