THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Paris Saint Germain amethibitisha kwamba Neymar anataka kusepa ndani ya kikosi hicho.
Tuchel amesema kuwa alifahamu ishu hiyo ya nyota huyo wa timu ya Taifa ya Brazil kutaka kusepa ndani ya kikosi hicho kabla ya michuano ya Copa America.
"Nilitambua wazo la nyota Neymar kutaka kusepa kabla ya michuano ya Copa America, ila linapokuja suala la maamuzi ni suala lake na klabu," amesema.
Neymar inaripotwa anataka kusepa na klabu anayofikiria kwenda ni klabu yake ya zamani ya Barcelona huku Juventus nao wakitajwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment