DAVID de Gea anatazamiwa kusaini kandarasi mpya ya miaka mitano kuendelea kuitumikia klabu yake hiyo huku mshahara wake ukizidi kutuna.
Mlinda mlango huyo hakuwa na hesabu za kuongeza mkataba mpya na iliripotiwa kwamba huenda angeibukia PSG.
Kwa sasa United inaelezwa kuwa imekubali kumlipa mshahara wa pauni 375,000 sawa na sh.bilioni moja kwa wiki.
Licha ya kuongezewa mshahara bado hajamfikia nyota namba moja wa kikosi hicho kwa kukunja mkwanja mrefu ambaye ni Alexis Sanchez anayekunja pauni 500,000 sawa na sh.bilioni 1.4 kwa wiki na amepachika mabao matano kwenye mechi 45 alizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment