July 3, 2019


UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa kwa sasa hauna mpango wa kusajili wachezaji kutoka nje ya nchi kutokana na kuamini uwezo wa wachezaji wa ndani.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa  klabu haina hesabu za kusajili nyota wa kigeni.

"Kwenye klabu yetu haitatokea tukasajili wachezaji wa kigeni, sura zao itakuwa ni ngumu kuonekana kwetu kwa kuwa tuna imani na wachezaji wa ndani.

"Kwa sasa tumeanza majaribio ya wachezaji wa ndani tukiwa na lengo la kusuka kikosi kipya hivyo tutawasili kwa kadri watakavyoonyesha uwezo wao," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Ruvu shooting bana msinlete poyoyo mambo ya kutokusajili nje 1. ni pesa, kumbukeni mlisema mnabana badeji, msitegemee wachezaji wa ndan wataleta upinzani hata kidogo kwa upande wa makombe, 2 kwa kuwa hawana malengo yoyote yale ya kombe tofauti na kukamilisha ratiba ya ligi 3 hawashiriki michuano yoyote ile ya nje ndani ni FA na ligi pekeee sasa kuna haja gan ya kuchukua wachezaji wa nje?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic