July 3, 2019


EVARIGITIUS Mujahukwi aliyekuwa mshambuliaji wa Mbao FC yenye maskani yake Mwanza amejiunga na klabu ya Kagera Sugar.

Kagera Sugar imenusurika kushuka Daraja msimu wa mwaka 2018-19 baada ya kuwa na matokeo ya kusuasua hali iliyoifanya ichezemchezo wa PlayOff na Pamba na kushinda kwa mabao 2.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mujahukwi amesema kuwa mchezaji hachagui kambi hivyo msimu ujao atakuwa kwenye changamoto mpya.

"Nimesaini kandarasi ya mwaka mmoja Kagera Sugar hivyo nitakuwa na klabu mpya msimu ujao kwa ajili ya kupata changamoto mpya," amesema.

Anakuwa mchezaji wa pili kusaini Kagera Sugar akiungana na Frank Ikobela ambaye naye tayari amemwaga wino.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic