TIMU ya Senegal haijawahi kutwaa kombe la Afcon na Ijumaa watakuwa na kibarua cha kumenyana na Algeria kwenye mchezo wa fainali.
Mara ya mwisho Senegal kutinga hatua ya fainali ilikuwa ni mwaka 2002 na muda huo kocha wao Alliou Sisse maarufu kwa jina la Rasta alikuwa akicheza nafasi ya kiungo mkabaji.
Imepita miaka 17 tangu watinge hatua hiyo ya fainali ya michuano hii mikubwa Afrika ambayo inafanyika nchini Misri na hii ni mara yao ya pili kutinga hatua ya fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment