July 12, 2019


MLINDA mlango wa Simba, Beno Kakolanya amesema kuwa kutokana na usajili ambao Yanga wameufanya msimu huu anaona kila dalili za ushindani mkubwa msimu ujao.

Kakolanya ambaye amesajiliwa na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga amesema kuwa kama wachezaji waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho watakuwa na uwezo kama ambao anausikia basi watatisha msimu ujao.

“Nawapongeza Yanga kwa usajili waliofanya msimu huu na unaonekana ni bora hivyo kwa harakaharaka inaonesha msimu ujao kutakuwa na ushindani, hivyo napenda kuwapongeza katika hilo,” amesema.

Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa ndani ya Yanga ni pamoja na mshambuliaji Juma Balinya, beki Ally Mtoni, Ally Ally, mlinda mlango Metacha Mnata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic