July 3, 2019



JACOB Massawe aliyekuwa nahodha wa Stand United amejiunga na Gwambina FC.

Massawe amejiunga na kikosi hicho kwa kandarasi ya mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Daraja la kwanza baada ya  timu yake ya Stand United kushuka daraja.

Wachezaji wengine ambao wamesajiliwa na Gwambina FC ni pamoja na Antonio Matogolo aliyekuwa Geita Gold, Raizin Hafidhi aliyekuwa Coastal Union, Ibrahim Isihaka kutoka Alliance, Malika Ndeule na Ibrahim Job ambao walicheza Ndanda FC.

Pia aliyekuwa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Kelvin Sabato amejiunga na timu hiyo kwa kandarasi ya miaka miwili.

1 COMMENTS:

  1. Turudi kwenye "vumbi letu na usajili wa magazeti na mihemko ya ushabiki wa timu za Kariakoo zinazodumaza soka letu"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic