July 3, 2019


WALTER Bwalya mshambuliaji wa Nkana FC ya Zambia amesema kuwa yupo tayari kusaini Simba iwapo watamhtaji.

Bwalya amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba na kuna taarifa kwamba amewaaga wachezaji wenzake kwamba anakuja Bongo kujiunga na Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.

"Sijafanya mazungumzo na Simba mpaka sasa na sijui kama wao wanahitaji huduma yangu, natambua kwamba Simba ni timu kubwa lakini hakuna dili yoyote kati yetu.

"Mkataba wangu wa miaka miwili ndani ya Nkana FC unaelekea ukingoni na nimebakiwa na miezi sita, sheria inatoa nafasi ya mimi kuzungumza na timu yoyote kama itatokea watakuja nitasikiliza ofa yao," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Hivi hata kingereza mnajua kweli!? Tuwekee hata clip basi ya kumuhoji!! Acheni porojo, mnaua soka letu kwa kujidanganya kisha mnalaumu makocha

    ReplyDelete
  2. Naona vijana wanapigana vikumbo kuufikia Simba

    ReplyDelete
  3. Usajili wenye mihemko na utashi wa mashabiki kuliko mahitaji ya kiufundi ya Kocha Aussems...sio kila mchezaji atafiti mfumo wa mwalimu.....hata kama tunampenda kiasi gani

    ReplyDelete
  4. Simba shida kubwa ni mabeki siyo washambaliaji. The Big problem in simba sports club is defenders not the strikers. So the coach chave to be careful

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic