SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limezitaka timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara pamoja
na zile zinazoshiriki Daraja la Kwanza kukamilisha usajili wake mapema kabla ya
dirisha la usajili kufungwa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Clifford
Ndimbo amesema kuwa hakutakuwa na muda wa kuongeza na zimebaki siku 10.
“Timu zote
zinapaswa zisajili wachezaji wao kisha zikamilishe na usajili wa mtandao ambao
ni Tanfootabll Connect kabla ya tarehe 31 ambapo dirisha litafungwa.
“Dirisha
likifungwa hakutakuwa na muda wa kuongeza kwani siku kwa sasa zimebaki chache
wanapaswa wakumbuke kutimiza majukumu yao," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment