July 21, 2019

ETTIENE Ndayiragije Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa leo watapambana kulipa kisasi mbele ya KCCA  katika mchezo wa fainali ya kombe la Kagame nchini Rwanda.

Azam na KCCA zilikuwa kundi moja ambapo katika mchezo wa hatua za makundi uliozikutanisha timu hizo Azam ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

"Awali tulifungwa kwa kuwa kikosi hakikuwa na muunganiko kwa sasa tumetengamaa na tupo tayari kwa ushindani.

"Tunakumbuka kwamba KCCA walitufunga katika hatua ya makundi, kwa sasa tumeimarika vizuri tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tunataka kulipa kisasi kwa kuwafunga na kutwaa ubingwa," amesema.

Azam ndio mabingwa watetetezi wakishinda leo watakuwa wametwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic