WABRAZIL SIMBA WAFICHWA
WAKATI usajili ukizidi kukolea ndani ya klabu ya Simba imebainika kuwa nyota wapya wa klabu hiyo Wabrazili tayari wamepelekwa kwenye hoteli ambayo Simba huweka kambi yao.
Wachezaji ni Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Vieira na Henrique Wilker da Silva.
Simba huweka kambi yake katika Hoteli ya Seascape iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam karibu kabisa na fukwe za Bahari ya Hindi.
Nyota hao awali walifikia sehemu tofauti ikiwemo Hoteli ya Sea Cliff ya jijini hapa mara ya kusaini mikataba yao mipya na klabu hiyo.
Habari za ndani kutoka ndani ya klabu zinadai kuwa, nyota wao wamepelekwa pale Seascape tayari kwa kusubiri wenzao ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu ujao.
Mchezaji mwingine aliyesajiliwa ni pamoja na Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman na mchezaji ambaye ameagana na Simba rasmi kimataifa ni James Kotei.
0 COMMENTS:
Post a Comment