WENGINE SIMBA KUTIMKIA AFRIKA KUSINI
WAKATI usajili ukizidi kushika kasi inatajwa nyota wawili wa kikosi hicho wanatarajia kujiunga na Klabu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Nyota hao wawili mmoja wapo ni beki na mwingine ni kiungo na kwa sasa wapo hatua za mwisho kukamilisha usajili wao. Taarifa za ndani zinadai kuwa klabu hiyo imevutiwa na wachezaji hao ndiyo maana zimeamua kuingia mazungumzo na nyota hao na mambo ya kikaa sawa wiki hii huenda wakasaini.
Wachezaji hao wanaotoka Simba mmoja ni kiungo na mwingine ni beki, Black Leopards na timu nyingine za huko zinavutiwa na wachezaji wa Simba baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.
“Simba kwa sasa imekuwa ‘hot’ kutokana na kile ambacho walifanya kwenye Ligi ya Mabingwa, ndiyo maana hata Black Leopards wamejitosa kusaka saini ya kiungo na beki kutoka kwenye klabu hiyo.
“Na taarifa za haraka tu mmoja wapo ni Paul Bukaba lakini huyo kiungo siwezi mtaja kwa sasa tusubiri kila kitu kiweze kukamilika,” kilisema chanzo.
Ataondoka mchezaji simba ikiwa tu wameamua aondoke.Kama waliweza kumzuia Ibrahim Ajibu kujiunga na timu yenye mkwanja matata kama mazembe basi mjue simba ya sasa sio mchezo.
ReplyDeleteHiyo ni Niyonzima na Juuko
ReplyDelete