July 8, 2019



MABINGWA wa kihistoria wa Tanzania Bara, Yanga leo wametimkia Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi.

Msimu wa mwaka 2019-20 unatarajiwa kuanza Agosti 23 na mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya Simba na JKT Tanzania uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa wamechagua Morogoro kutokana na utulivu.

"Timu leo imeelekea Mrogoro kwa ajili ya kambi na itakuwa huko mpaka msimu utakapoanza, tumejipanga kufanya vema msimu ujao ndio maana tunakwenda kuweka kambi sehemu tulivu," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Naona Yanga wanapaua kikosi

    ReplyDelete
  2. Naona Yanga wanapanua kikosi

    ReplyDelete
  3. Kwanza ilikuwa nje ya nchi au ndio kupunguza matumizi

    ReplyDelete
  4. Kambi ni popote tu pale penye utulivu inatosha sio lazima Nchi za nje

    ReplyDelete
  5. Ndugu yangu nje utapata timu za kujipima zenye uwezo wa hali ya juu ikusadie kwenda kupambana na timu zenye viwangi kuliko kujipima na timu za chini ya minazi

    ReplyDelete
  6. hela hakuna kwahiyo morogoro panatosha. Poleni watani

    ReplyDelete
  7. Ni bora Hukohuko Moro kuliko kupoteza hela ambayo tunaihitaji kulipia mastaa wetu. Tusifanye kwakuwa watani wamefanya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic