MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba zawadi zao bado zinashughulikiwa kwani mpaka sasa bado hawajapewa.
Simba ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2018-19 na msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 23 watakuwa ni watetezi.
Wlfred Kidao Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa suala la zawadi kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara bado linafanywa kazi.
"Bado tunafanyia kazi kuhakikisha tunatatua changamoto hii iliyojitokeza baada ya kukosa mdhamini mwaka jana," amesema Kidao.
Madudu yanaendelea
ReplyDeleteHii ni Aibu tena kubwa. Kumbuka Simba ni mchanganyiko wa wachezaji na makocha wa matalfa mbali mbali nadhani wageni wanatushangaa sana. Na nadhani wanawashngaa Simba kwa kuhangaika na kuupigania mchezo wa mpira wakati wahusika wakuu wanaopiganiwa hawajali. Hapa nazungumzuia zaidi wizara inayoshughulikia michezo kwa maana ya serikali pia. Kama chama cha mpira kimeshindwa kuwa na wadhamini hadi kufikia kushindwa kumzawadia bingwa wa ligi kuu ya nchi,wizara husika ilichukua hatua gani? Hatuoni hii kuwa ni aibu ya nchi na si ya TFF au Simba? Katika hali hii kweli tunathubutu kutamani kuona kuwa tuna timu imara kimataifa? Hata sudani kusini bingwa wa ligi yao haondoki bila ya zawadi. Sisi watanzania vipi lakini?
Delete