BAGHDAD Bounedjah bao lake la dakika ya pili limetosha kuipa timu ya Algeria ubingwa wa Bara la frika kwa mwaka wa 2019 nchini Misri dhidi ya Senegal ambao hawajaambulia hata bao.
Algeria wanaibuka kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Senegal kwenye michuano iliyomalizika nchini Misri.
Hii inakuwa ni baada ya miaka 29 kupita hatimaye Algeria wanatawazwa kuwa mabingwa wa Afrika.
Mara ya kwanza kufanya hivyo ilikuwa mwaka 1990, wametwaa kombe hilo bila kupoteza mchezo hata mmoja.
Sadio Mane wa Senegal, Cedric Bakambu wa Congo na Adam Ounas wa Algeria pamoja na Mahrez wenye mabao matatu wanakikosa cheo cha mfungaji bora mwaka huu.
ReplyDelete