KIKOSI cha Azam FC, kinatarajia kuondoka nchini kuelekea Ethiopia, kesho Jumatano saa 10 alfajiri kwa ajili ya kuiwahi Fasil Kenema kwenye mchezo wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Bahir Dar Jumapili saa 10.00 jioni.
Msafara wa Azam FC utaondoka na wachezaji 23,watano wa benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije pamoja na viongozi na maofisa wa timu hiyo.
Aidha katika kukabiliana na changamoto za ugenini, Azam FC ilitanguliza sehemu ya uongozi wake tokea juzi wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', ili kuandaa mambo mbalimbali na taratibu zote za timu ikiwa huko.
Mabingwa hao wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports watakaoondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia, wamejipanga vilivyo kufanya vema kwenye michuano hiyo msimu huu, ikiwa na malengo ya kufika hatua ya makundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment