August 17, 2019


Sikia nikwambie brother..! Watu wengi sana ambao huwa WANAFURAHIA ANGUKO la WENZAO ama wanatamani KUFELI kwa WENGINE huwa wanakuja kukutana na ANGUKO LA AIBU kwenye maisha yao.
.
Unakuta mtu anapanga njama kumfanya mtu mwingine achukiwe na bosi wake.Unakuta mtu anaweka mpango wa siri ili kukatisha NDOTO ZAKO, kuna watu wanathubutu hata kupanga mbinu ya KUMWANGUSHA au KUMCHAFUA mwingine wakiamini hiyo itawasaidia,lakini mwisho wake wanagundua aibu inawakaribia.
.
Moja ya Kitu ambacho unatakiwa kujifunza kwenye maisha ni KUFURAHIA MAFANIKIO YA WENGINE,KUSHEHEREKEA KUINULIWA KWA WENGINE na KUTAMANI KUNG’ARA KWA WENGINE.
.
Kwa taarifa yako HAKUNA mwenye UWEZO wa KUCHUKUA nafasi YA mwingine,(kuwa kama yule) anaweza kujaribu kwa MUDA mfupi tu lakini kuna kitu kitatokea na ATAIPOTEZA.Kama vile ambavyo Kila NYOTA INA SEHEMU YAKE MAWINGUNI na kila mmoja inang’aa kwa NAMNA yake, vilevile kila mtu ni “STAR” kwa namna yake, Waombee wengine mema na mafanikio, MUNGU atakurudishia MARADUFU.
.
Nakuombea MUNGU aendelee kukufanikisha KINYUME na wanaotamani ANGUKO LAKO.
.
USIHANGAIKE KUZIBA NYOTA ZA WENGINE ZISIN’GAE,HANGAIKA KUIFANYA YA KWAKO ING’AE ZAIDI.

Na Dismas Ten

3 COMMENTS:

  1. Sishangai yanayotokea Yanga kwenye mechi za kirafiki na za mashindano ya CAF nilishashauri huko nyuma kuwa Yanga inahitaji kuliimarisha benchi la Ufundi kuongeza ujuzi na mbinu kwani viwango vya wachezaji vinaporomoka kwa kiwango cha juu mno....uwezo wa benchi la ufundi la Yanga ni mdogo mno...na kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuliimarisha benchi la ufundi kuna hatari sana huko mbele aibu itatokea...Mimi si tu kwamba ninatathmini mchezo wa soka kwa umahiri ninazichambua timu kutokana na mechi zinazocheza.....nilisema kuwa Yanga inahitaji kuiiga Simba kutafuta Kocha Msaidizi kutoka Ulaya au Hata Amerika Kusini au Asia au Hata Africa mwenye viwango vya FIFA....ili wachezaji waongezewe mbinu katika mashindano.....Bado Yanga wana wachezaji wazuri lakini soka wanalocheza watapata tabu wakicheza na timu zenye mbinu za kubadilisha mchezo haraka.....kwahiyo hili la kubadilisha au kuliimarisha benchi la ufundi haliepukiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ayo ni maoni yako,but unaposema benchi la ufundi Lina uwezo mdogo sijui umetumia kipimo kipi kupima uwezo wa benchi la ufundi la yanga kwa mda huu mfupi! Unapima uwezo wa benchi la ufundi kwa mechi moja ya kimataifa na mechi za majaribio au? Nina mashaka na uelewa wako wa masuala ya soka, sababu mpaka sasa ujui kinachoisumbua yanga ni kitu gani na sidhani Kama umefatilia mechi zote za yanga iwe za majarbio au ile ya mashindano, kutengeneza combination ya time iliyosajili 95% ya wachezaji wapya sio suala la kuamka asubuhi na kufanikiwa siku iyo iyo ni suala la mda, uyo uyo zahera unaemponda Leo kwamba Hana uwezo ndo uyo uyo aliibuka kuwa kocha Bora mara mbili msimu uliopita inakuwaje Leo hii unasema benchi la ufundi Alina uwezo? kwa kuwa timu imedroo na township rollers? Unaweza kuniambia kwenye kikosi kilichocheza na township ni wachezaji wangapi waliokuwepo msimu uliopita walianza kikosi Cha Kwanza? Ni wawili tu waliobaki walikuwa wapya je wamekaa pamoja kwa mda gani ili kutengeneza mfumo wa kucheza kitimu? Mda mwingine watanzania hasa mashabiki uwa wanataka Mambo yatokee kwa haraka Kama vile kupika ugali na kuiva mda huo huo ni Jambo ambalo aliwezekani ktk soka mpira una njia zake na sio kukurupuka, zahera tunayo imani nae Sana na mbaya zaidi wanaopiga kelele ni upande wa pili,iyo inaonyesha zahera ni kiboko yao na kwa timu aliyoisajili mje mumuhukumu mwisho wa ligi nafikiri Kila mmoja atakuwa na jibu!

      Delete
    2. Acha visingizio benchi la Yanga ni bovu ni la kawaida sana huwezi kulinganisha na Simba au As Vita au Al Ahly

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic