HARUNA
Shamte, beki mpya wa Simba, mtaalamu wa mipira iliyokufa ambapo msimu uliopita
alifunga jumla ya mabao 5 akiwa Lipuli na sasa amesaini kandarasi ya miaka
miwili ndani ya Simba amesema ana imani leo wanabeba ngao ya jamii mbele ya Azam
FC.
Azam FC na Simba leo zitakuwa kazini kufungua pazia
la Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23 kwa mchezo wa ngao ya jamii
uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Shamte amesema kuwa wanatambua wapinzani wao Azam FC ni
bora ila bado ubora wa kikosi cha Simba unawapa ushindi.
“Hakuna
ambaye hatambui ubora wa kikosi cha Azam FC ndani ya timu ya Simba kwa sasa ila
linapokuja suala la kikosi kipana kipo ndani ya Simba na hayo yataonekana
uwanjani.
“Kila sekta
kwa sasa imekamilika ni kikosi cha moto, mbinu za Kocha pamoja na ushirikiano
uliopo ndani ya kikosi tuna imani ya kubeba ngao mbele ya wapinzani wetu,”
amesema.







0 COMMENTS:
Post a Comment