August 31, 2019


MBWANA Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgij kesho timu yake itakuwa na kazi ya kufanya mbele ya wapinzani wao Club Brugge. 

Ligi yao imezidi kupamba moto ambapo wamecheza jumla ya michezo mitano huku Samatta akipachika jumla ya mabao matano matokeo yao mechi za mwanza yapo namna hii:-

 Genk 2-1 Kortrijk

Benjamin Nygren dk 59, Ianis Hagi dk ya 76 walicheka na nyavu kwa upande wa Genk huku wapinzani wao Kortrijk wakiandika bao kupitia kwa Julien De Sart dk 13.

Mechelen 3-1 Genk

Waliopeleka kilio Genk ni William Togui dk ya 18
Gustav Engvall dk ya 77 na Igor de Camargi dk ya 80 na lile la Genk likipachikwa na Samatta dk ya 45.

Genk 0-2 Zulte Waregem

Mabao ya maumivu kwa Genk yalifungwa na Henrik Bjordal dk ya 6 na Saido Berahino dk ya 78.

Waasland-Buveren 0- 4 Genk, Joseph Painstsil 21 alifungua lango kabla ya Samatta kuangamiza kabisa kwa kutupia hat trick yake ya kwanza dk ya 52, 66 na 85.

Genk 1-0 Anderlecht maumivu kwa wapinzani yalisababishwa na Samatta dk ya 55.

Genk ipo nafasi ya 6 ikiwa imecheza jumla ya michezo mitano imejikusanyia pointi 9 na kinara ni Standard Liege mwenye pointi 12 huku wapinzani wao watakaomenyana nao kesho wakiwa nafasi ya nne wamejikusanyia pointi 10 wakiwa wamecheza michezo minne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic