BRUNO Tarimo, maarufu kama Vifua Viwili, leo atakuwa na kazi moja ulingoni kupeperusha
Bendera ya Tanzania kwenye pambano la raundi 12 dhidi ya Mserbia, Scheka Gurdijeljac.
Pambano hilo
la ubingwa wa Dunia linatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na rekodi za
Vifua viwili kutopoteza pambano zaidi ya kupoteza moja kwa pointi kati ya mapambano 26
aliyocheza.
Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa leo Agosti 31 nchini Serbia ukumbi wa Hala Pendik Novi Pazar.
Akizungumza
na Championi Jumamosi Vifua Viwili
alisema kuwa :“Natambua
kuwa watanzania wananiombea nitapambana kubeba ubingwa ili kupeperusha vema
Bendera ya Taifa kikubwa sapoti kwani maandalizi yapo vizuri,” alisema Vifua
Viwili.
0 COMMENTS:
Post a Comment