August 24, 2019


HATIMAYE uhakika wa taarifa za kuwa mkali wa Kwangwaru Harmonize hayupo tena katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) umethibitishwa na meneja wa kimataifa wa Diamond Platinumz, Sallam SK.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Harmonize amejitoa katika Lebo ya WCB lakini palikosekana mtu wa kuthibitisha taarifa hizo.

Akizungumzia ishu hiyo, Sallam SK alisema: “Ni kweli Harmonize ameandika barua ya kuomba kujitoa katika Lebo ya Wasafi , hivyo sisi kama uongozi hatujaona kama hilo ni tatizo kwa sababu mwisho wa siku hauwezi kumzuia mtu kufanya kile ambacho anaona kwake kina manufaa zaidi.

2 COMMENTS:

  1. Mimi Nahisi Harmonize Akijitoa Lazima Atapoteza Mwelekeo Kimziki Anaimba Vizuri Ila Lebo Ya WCB Ilimfanya Awe Juu Zaidi Na Kuna Watu Wengi Wanao Ishabikia Lebo Na Msanii. Rich Mavoko Yuko Wapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kila binadamu ana hulka yake na huwezi kumpa lawama za kujiondoa bila kujua upande wa pili wa shilingi inafananaje.Hawezi kutueleza kwani pengine mkataba unambana asitoe siri.mwisho wa siku ni muda tu utaamua na ni vizuri kwa sisi hasa wanaume kumtakia kheri ya mafanikio anachokusudia kukifanya....InshaAllah

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic