August 27, 2019


Aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa kikosi cha timu hiyo juzi kiliingia kucheza na UD Songo wakiwa na matokeo ya msimu uliopita.

Julio amesema kuwa wachezaji wa kikosi hicho waliingia wakijiamini kwa kuichukulia Songo kama timu ya kawaida lakini badala yake ikapelekea kutolewa kwenye mashindano.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa, Simba na Songo walimaliza mechi kwa matokeo ya 1-1 yaliyokuwa na faida kwa wapinzani ambao walisalia kwa faida ya bao la ugenini.

Aidha, mbali na kusemea hilo, Julio amesema pia hakuna wachezaji kutoka Brazil wanaoweza kuja Tanzania kwa ajili ya kucheza soka.

Ameeleza kuwa wabrazil watatu waliosajiliwa wamekuja kwa ajili ya upigaji na kutalii na akieleza kuwa kuna watu watakuwa wamekula pesa.

"Hakuna mbrazili anayeweza kuja kucheza soka Tanzania.

"Watu wa huko wana malengo ya kucheza soka la mbele zaidi, hao wamekuja kutalii tu na si wachezaji mpira, subiri mtaona." 

7 COMMENTS:

  1. Nafikiri kwenye hili kuna haja ya Mo Dewji kuwashughulikia walio muingiza mjini, kweli hao wabrazili wasipo onyesha ubora wao hakuna jinsi walio husika kuwaleta kweli inabidi wachunguzwe na kama kuna upigaji waadhibiwe fasta, hawa hawakua chaguo la mwalimu ndio maana kawaweka kando na pia uwezo wako hauja mridhisha.

    ReplyDelete
  2. Kama mtu kacheza under 20 ya brazil hawezi kuwa mbaya.Ausems mwenyewe ni tatizo kubwa ni mwoga, anakariri na hatoi nafasi kwa wachezaji kuonyesha uwezo wao. Ukitaka kujua Ausems angalia issue ya Manula vs Beno

    ReplyDelete
  3. Nilijua iko siku Julio ataibuka na kuponda usajili wa Simba.Tatizo la Julio ni kila la kwake analosema au analotaka basi likubalike.Nitamshangaa sana kocha alipowapa ripoti viongozi kuwa anahitaji wachezaji wa aina hii na kuletewa wachezaji ambao yeye hakuwadhitisha?Basi kama ni hivyo kocha anapaswa awajibike maana hajiamini na ni kama ameuziwa mbuzi kwenye gunia? Sikatai kuwa hawo wabrazil wa Simba pengine hawana viwango bora lakini napingana na kauli yake ya kusema kuwa hakuna mbrazil anayeweza kuja kucheza soka Tanzania kwa kuwa eti wabrazil wana malengo ya mbali.Pengine aelewe kuwa Brazil kuna watu milioni 250 kwa mujibu wa sensa ya miaka kumi iliyopita.Mchezaji toka Brazil kwenda kucheza Europe ni lazima awe anatoka kwenye klabu inayocheza daraja la kwanza na kwa maana hiyo haiwezakani mchezaji wa daraja hilo aje Tanzania labda kwenye vilabu tajiri Africa kama Morocco, Misri n.k.Mchezaji mbrazil anaweza akawa kwenye kiwango bora toka daraja la pili au tatu na akaja Tanzania akapeform vizuri sana na hii ni kwa sababu kwao Brazil wachezaji ni wengi sana na wana viwango lkn hawaonekani na uelewe pia maisha ya wabrazil ni ya kawaida maana kuna tabaka kubwa la matajiri na maskini pia dili za upigaji na rushwa ndio maisha kwao.Hivyo nao kama kina Viera Fraga wanahaha kutafuta maisha nje ya Brazil ili wapate mkate wao.Hata hapa nyumbani kuna wachezaji wazuri wako timu za daraja la chini na tunawaona kwenye ndondo na wanaondoka kwenda nchi za nje kucheza soka na hawatoki kwenye vilabu vya Simba au Yanga na hata watoto wake Julio wanacheza mpira nje na hawajawahi kuchezea vilabu vya ligi kuu Tanzania.Kuna wachezaji wengi wa kibrazil wanacheza soka nchini Angola, South Africa, Tunisia, Morocco na wengine walipata kucheza Morocco na wakabadili uraia ili wacheze timu ya Taifa.Lakini yote ni swala la muda utatueleza na muhimu ni kuweka akiba ya maneno.

    ReplyDelete
  4. Julio ni mchumia tumbo,maneno mengi mdomoni halafu kumbe anapumuliwa

    ReplyDelete
  5. Ifike mahali watu tuweke ushabiki kando katika wale wabrazili kuna beki na viungo mechi ya juzi hakuna asiyejua kama mkude na shiboub walipotea kabisa then coach anamtoa shiboub anamuingiza miraji
    Miraji anaingiaje kubadili matokeo wakati kuna wabrazil!?? Hapa ndio pana ukakasi zaidi timu inahitaji matokeo mwalimu anafanya sub ya beki
    Mechi ngumu kama ile unafanya sub3 zote za wazawa na una wabrazil ktk benchi hii haingii akilini ndio maana kina julio wanahoji

    ReplyDelete
  6. Watu wamepiga hela kwa wabrazil. Waliwaona wapi wanacheza bwana? Tag Magoly

    ReplyDelete
  7. Kocha Simba ni tatizo kubwa sana.Timu yenye wachezaji bora kama hii, makocha wanaitamani waweke CV za nguvu,ila huyu ameshindwa kuitumia.
    Tutalalamika waBrazil mara mchezaji Fulani au yule n.k. Lakini tatizo ni Mzungu hana mbinu wala upeo. Makocha wengine wanatimu mbovu sana lakini mbinu zao zina saidia kupata ushindi ingawa mwembamba. Je wangepata usajili na timu bora kama Simba? Simba ijaribu kumbadili mtaona matokeo.
    Shida ni kuwa Simba ikiwa na wachezaji bora na fedha yakutosha, huwa inakosa kocha bora. Ninawakumbuka wale makocha akina Elias, wale wa Serbia n.k. lakini walikuta club masikini na wachezaji wakiwango cha chini. Kama makocha hao wange ikuta Simba hii, kombe LA Africa tungekuwa kama mara tano mfululizo tuna fika nusu au finalist kama Simba kuchukua kombe kabisa.
    Ila kwa Ausens Mimi nasema hatuendi kokote zaidi ya kubahatisha tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic