August 6, 2019


MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba, leo ameibuka shujaa kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo ya Zambia baada ya kupiga 'hat trick' wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya mabingwa hao mara 7 kutoka Zambia.

Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni hitimisho la kilele cha SportPesa Simba Wiki ulihudhuriwa na mashabiki wengi huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim ulikuwa na ushindani kutokana na kila timu kutafuta ushindi kwa hali na mali.

Kagere alianza kucheka na nyavu ndani ya Uwanja wa Taifa dakika ya 3 baada ya mlinda mlango wa Power Dynamo kujichanganya na kutoa pasi iliyomkuta Kagere ambaye hakufanya hiyana na akarejea tena kucheka na nyavu dakika ya 58 akimalizia pasi maridadi iliyopigwa na Deo Kanda kabla ya kukomelea msumari wa mwisho dakika ya 77.

Bao la kufutia machozi kwa Power Dynamo lilipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 24 na liliwekwa kimiani na Jimmy baada ya mabeki wa Simba kujichanganya kuokoa kona iliyopigwa na wapinzani.

Kipindi cha pili Simba walichangamka na Miraj Athuman alikosa bao la wazi dakika ya 78 baada ya Mohamed Hussein 'Tshabalala' kuachia pasi sukari iliyoshindwa kujaa vizuri mguuni mwa Miraji na Clatous Chama naye dakika ya 80 alikosa bao la wazi baada ya kupigiwa pasi sukari na Meddie Kagere. 

Kagere amesepa na mpira wake leo baada ya kufunga 'hat trick' yake ya kwanza leo uwanja wa Taifa baada ya Ligi kuu kumalizika na inatarajiwa kuanza Agosti 23.

5 COMMENTS:

  1. Maandamano hayakuleta ushindi. Ushindi umeletwa Kwa ukarimu Kwa wagonjwa wenye mahitajio wa Ocean Road Hospital na haya yataigwa baadae

    ReplyDelete
  2. Dah! Harus Ya Simba Imeenda Vizur Sana Lakini Send Off Za Vyura Ilikuwa Mbaya ,

    ReplyDelete
  3. Mikia itakunjwa muda c mrefu dynamo wenyewe matutusa tu.

    ReplyDelete
  4. Ipi ngumu Dynamos, Kenya au Sharks au za Moro alafu ndio umkunje mkia Mnyama

    ReplyDelete
  5. Kariobangi Sharks walifungwa na KMC nä nyie mpaka mlibebwa kwa goli la tuta.Ingizeni timu tarehe 4 Januari halafu msipaki basi mkifungwa 4 mmecheza sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic