KARIA AJA KAULI KALI KUHUSU NEMBO YA VODACOM, ATAKAYEBADILI RANGI KUPIGWA CHINI
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema hakuna timu yoyote itakayoruhusiwa kubadili rangi ya nembo ya mdhamini katika jezi.
Kauli hiyo imekuja kufuatia sintofahamu ya nembo ya mdhamini mkuu ambaye ni Vodacom na Yanga kubadilishwa misimu kadhaa nyuma na kuwa ya kijani.
mambo yameonekaka kuwa tofauti kwa msimu huu na sasa rangi ambayo itatumika kwa timu zote itasalia kuwa ileile nyekundu.
Karia amesema hatua za kisheria kwa atakayebadili rangi ya mdhamini zitachukuliwa.
"Mkataba wetu wa udhamini una masharti yake ambayo tunatakiwa kuyafuata na hatutoruhusu yeyote kwenda kinyume nayo.
"Masharti hayo ni kama kitabu cha msahafu na kila mmoja anapaswa kuyafuata. Yeyote ambaye hatoyafuata tutamtoa kwenye familia yetu," amesema Karia.
Tunatakiwa kwenda na wakati.Mambo ya wazee kina Kilomoni na Akilimali wanapaswa waelewe kuwa kila zama na kitabu chake.Nembo ya mdhamini haichezi mpira.Wakati Rais wetu wa sasa anaipeleka Tanzania kwa mwendo wa kasi inabidi sote twende na kasi hiyo na hakuna kubembelezana kwa issues za kutuletea maendeleo hata kama watakaofaidika ni vizazi vijavyo.Klabu hazipaswi kungojea fadhila (wafadhili) bali zinahitaji wawekezaji ili wafanye biashara kwa manufaa ya klabu na mwekazaji.Hatuhitaji wafadhili ambao wamepita wengi sana ndani ya vilabu vyetu lkn ni maendeleo gani wameachia klabu zetu?Mfadhili anakuja na anafadhili na kuondoka anavyojisikia lakini mwekezaji hawezi kufanya mambo anavyotaka kwani kuna sheria zitakazombana.
ReplyDeleteKweli hiki muhimu kwa maslahi ya mdhamini. Tuna mpira kila timu iwe na uwezo wa kushindana
DeleteAcheni unafiki kwani mwaka jana tulikua na mdhamini?mbona tulicheza
ReplyDeleteUwe una fikir ndo una andika sawa
DeleteAcha unafiki ligi haikua na mdhamini na mlicheza waliokua na pesa kama azam na Tim nyingine ndo hawakuona shida je tim kama stend United hukuona zilivyotaabika kutokana na ukata wa fedha? au unachozungumzia wewe ni ushabiki usiokua na maana
ReplyDeleteInaelekea hujaelewa chochote hapo kwenye hii habari
DeleteWadau ambao ni vilabu je walishirikishwa kabla ya kuingia mkataba na mdhamini?
ReplyDeleteMkuu washirikishwe kwan wao ndo wenye ligi au wanajua hata zawadi ya ligi inatoka wap
DeleteKaria una upeo mdogo wa elimu ndugu yangu huo mkataba wako wenye manufaa na wewe huwezi kuulinganisha na kitabu kitakatifu chenye maneno ya Mwenyezi Mungu "Quraani" bora tafuta mfano mwengine utowe
ReplyDeleteWewe unakunya na kuchamba,umejaza mavi tumboni unafananisha mkataba wako na msahafu boya wewe
ReplyDeleteMimi namuunga mkono ndugu Karia mkataba wa mdhamini uheshimiwe .safi sana
ReplyDeleteShida mtu akiwa na smartphone anajiona ana akili.....Watu wanapenda club badala ya kupenda mpira....hawataki kujifunza wenzetu duniani wanafanyeje.....Mashabiki wengi wa hizi timu za urithi upeo wa kufikiri ni mdogo sn
ReplyDeleteKm vp wasitupe pesa zao..lkn nembo nyekundu kwenye jezi zetu haikubaliki asilani.
ReplyDeleteSheria za mikataba ziheshimiwe. Uwez kuwa na kampun ya viatu then ukaweka nembo ya tikiti
ReplyDelete