YUSUF Ndikumana, nahodha msaidizi wa kikosi cha KMC amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wanakwenda kupambana nchini Rwanda.
KMC itamenyana na AS Kigali Agosti 10 ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kimataifa kabla ya kurudiana na wapinzani hao Dar kati ya Agosti 23-25.
"Tumejipanga vizuri na maandalizi yapo sawa, kwa sasa tunaamini kwamba tunakwenda kucheza mchezo kwa ajili ya Taifa hivyo hakuna kitakachoshindikana hata kama tutakua ugenini.
"Kwetu sisi kipaumbele kikubwa ni ushindi kwa kuwa mazingira sio changamoto kwetu hivyo mashabiki watupe sapoti," amesema.
Kila la kheri
ReplyDelete