LIOYD Kelly, kinda anayekipiga Bournermouth mwenye umri wa miaka 20 anapewa nafasi kubwa ya kufanya makubwa kwenye Ligi Kuu England ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Ijumaa.
Mechi ya kwanza itawahusisha Liverpool na Norwich City. Ni miongoni mwa mabeki ghali ambaye amekamilisha dili lake kwa dau la pauni milioni 13 akitokea klabu ya Bristol City mwanzoni kabisa mwa msimu.
Anaingia kwenye rekodi ya nyota saba wa gharama ambao wamemwaga wino ndani kikosi hicho cha Bournermouth.
Raia huyo wa England anakipiga pia kwenye timu ya Taifa chini ya miaka 21 anauwezo wa kucheza kwa akili na kujituma akiwa ndani ya uwanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment