August 1, 2019

SAID Maulid, Kocha wa timu ya Vijana chini ya miaka 20 wa Yanga, amesema kuwa tatizo kubwa la wachezaji wa timu ya Taifa wanashindwa kutumia mbinu ya ziada pale mpango wa mwalimu unapofeli.

Maulid amesema kuwa uwezo wa kushinda mbele ya timu ya Kenya ulikuwa mikononi mwa wachezaji wenyewe jambo waliloshindwa na kuongeza ugumu wa kupata matokeo.

"Wachezaji walikuwa wameshindwa kutumia uwezo binafsi baada ya plan ya mwalimu kushindwa licha ya kucheza kwa kujituma mwanzo mwisho.

"Sehemu pekee ambayo ilikuwa ina kazi ngumu ilikuwa ni sehemu ya ulinzi ambayo ilikuwa ina maelewano, katikati mipira ilikuwa inapotea na wakati mwingine viungo walikuwa wanarudisha nyuma mipira jambo lililokuwa linawapa kazi washambuliaji kutafuta mipira.

"Kuelekea mchezo wa marudio ni lazima wachezaji wawe na mbinu mbadala na kutazama namna gani ya kupeleka mashambulizi mbele na sio kutegemea plan ya mwalimu pekee," amesema.

Stars ilikubali sare ya bila kufungana na Kenya uwanja wa Taifa, Agosti 4 wataruduiana na Kenya nchini Kenya ili kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Chan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic