August 6, 2019



MCHEZO wa kirafiki wa kimataifa kati ya Simba na Power Dynamo uwanja wa Taifa umemalizika kwa Simba kuibuka wababe kwa ushindi wa mabao 3-1.

Bao la kwanza kwa Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 3 akimalizia pasi ya mlinda mlango wa Power Dynamo akaongeza bao la pili dakika ya 58 akimalizia pasi ya Deo Kanda na amepachika bao la tatu dakika ya 77

Kwa upande wa Power Dynamo wao walifunga bao dakika ya 24 kupitia kwa Jimy baada ya mabeki wa Simba kujichanganya.

13 COMMENTS:

  1. Mwaka wetu huu wataisoma kama ilivyo

    ReplyDelete
  2. mwaka wenu huu hooo! mikia f.c

    ReplyDelete
  3. wekeni takwimu sikwenye mechi ya vyura muliweka

    ReplyDelete
  4. Mnyama kashinda kwakuwa na jezi nzuri au kuwaziba bingwa WA magoli ya Mrogoro?

    ReplyDelete
  5. Sasa mngojeeni Ajibu walio jaribu Kwa kila njia asirejee kwao na huku Michael akitaka kulinda heshima yake

    ReplyDelete
  6. Deo Kanda(7), Shibob (8) Gereson (4) T - Santos, Kahata (25) Miraji Athumani = Simba = Kiujumla Nihabari Nyingine.

    ReplyDelete
  7. Kiza kimetanda Simba kaizima dainamoo kawaacha mabingwa WA Morogoro vinywa wazi na huku KMC akionesha jeuri yake. Huu utakuwa msimu WA vituko

    ReplyDelete
  8. Simba hata power Dynamo wameonyesha mchezo safi kabisa high standard of football kwakweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Simba walitulia.
    Mpira mkubwa umepigwa kipindi kirefu sijaiona timu ya Tanzania ikitawala mechi zidi ya timu ngeni hasa ukichukulia timu yenyewe inatoka Zambia. Hongereni sana Simba.

    ReplyDelete
  9. Ile Simba kujipima kwa timu zenye uwezo wa hali ya juu kuliko ilivo wenyewe ndio iliyoiwezesha kufikia kiwango ambacho wengi wasingesadiki juu ya kuwa watano WA kikosi hicho waliokuwa na timu ya taifa walipumzishwa na wengi walioshiriki Ni wapya. Kushinda Kwa watani imetokana na timu walizochaguwa kujipima nazo si timu ndogo za mitaani zisizo na uwezo wowote na kila wanapopata magoli magazeti yakisifu na kuipaza timu juu Ni kama vile kuwahadaa au kuwacheka badala ya kuwapa ukweli. Ukitaka kujipima kama unao uwezo wa kubeba kilo arbaini basi ujipime Kwa kubeba kilo Hansini na wala si kilo ishirini na hivi sasa ndio wapo Zanzibar wakijipima na timu wanahakika watazishinda.

    ReplyDelete
  10. Ilikuwa Jambo la mana kujima na timu zenye uwezo kama vile Azam, Mtibwa au KMC lakini inaonesha ikiogopa kushinda kupelekea kuvunjika moyo Kwa mashabiki mapema kabla ya kuanza msimu mpya au Township ya Botswana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic